Bahi
Mwenyekiti wa Kamati: Bw. Nicholaus William Iringo |
Katibu Msaidizi: Bw. Edward Mlinda Burton |
____________________________ Mawasiliano: ____________________________ TSC Bahi; Mtaa wa Kichangani, Kata ya Bahi; S.L. P 2993 Dodoma; Baruapepe: as.bahi@tsc.go.tz Simu: 026-2322402-4 |
Kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu, Wilaya ya Bahi
Bahi ni wilaya inayopatikana katika mkoa wa Dodoma nchini Tanzania. Upande wa kaskazini inapakana na Wilaya ya Chemba, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Dodoma/Jiji la Dodoma, Upande wa Kusini inapakana na Wilaya ya Chamwino na upande wa Magharibi inapakana na Mkoa wa Singida. Ofisi ya TSC Wilaya ya Bahi ni moja kati ya Ofisi saba (7) za Tume zilizopo katika Mkoa wa Dodoma.
Taarifa za Ofisi
Ofisi hii inahudumia Walimu katika Halmashauri moja (1) ambayo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Hadi kufikia Mei 2022, Wilaya ya Bahi ina jumla ya shule 72 za Msingi na shule 22 za Sekondari za Serikali. Kati ya shule 22 za Sekondari ni shule moja tu ina kidato cha tano na sita. TSC, Wilaya ya Bahi, kwa mujibu wa taarifa za walimu (Tange) kwa mwaka 2021/2022, inahudumia jumla ya Walimu 1031, Walimu 699 (396 Me, 303 Ke) ni wa shule za Msingi na walimu 332 (232 Me na 100 Ke) wa shule za Sekondari, waliopo kwenye Utumishi wa Umma.
Majukumu
Majukumu yanayotekelezwa ni kama yalivoainishwa kwenye Kifungu Na.12 cha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na. 25 ya Mwaka, 2015.
Masuala yalitekelezwa
Katika Mwaka wa fedha 2021/22, Walimu 28 waliajiriwa, (20 Msingi na 08 Sekondari), Walimu 53 walithibitishwa kazini (37 Msingi na 16 Sekondari), Walimu 64 walipandishwa vyeo, (42 Msingi na 22 Sekondari). Walimu 58 walibadilishiwa vyeo baada ya kujiendeleza kielimu, (47 Msingi na 11 Sekondari). Walimu 24 wana vibali vya ruhusa ya masomoni, wakiwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini. Walimu 08 wamepewa vibali vya kustaafu na walimu 03 wamestaafu.
Katika Mwaka wa fedha 2021/2022, Mashauri ya Nidhamu 04 yalifunguliwa na yote 04 yalihitimishwa. Katika uamuzi wa Mashauri hayo Walimu 03 walifukuzwa kazi na mwalimu mmoja (01) alipewa Karipio. Hakuna rufaa zilizotumwa.
Utawala
Ofisi ya TSC Wilaya ya Bahi inasimamiwa na Katibu Msaidizi ambaye ni Mtendaji wa majukumu ya Tume katika ngazi ya Wilaya.
Uongozi
Kwa mujibu wa Kanuni ya 46 (1) ya Kanuni za Tume ya Utumishi wa Walimu za Mwaka, 2016 Kamati ya TSC Wilaya ya Bahi inaundwa na Mwenyekiti, Wajumbe wanne (4) ambao ni Katibu Tawala wa Wilaya, Afisa elimu kutoka ofisi ya Idara ya Elimu Msingi, Mwakilishi wa Walimu wa shule za Msingi na Mwakilishi wa Walimu wa shule za Sekondari. Katibu wa Kamati ni Katibu Msaidizi wa Wilaya.
Kalenda ya Matukio/ Vikao
Vikao vya Kamati za Wilaya
Kuna vikao vinne vya kisheria kwa Mwaka kwa kila robo na katika mwaka 2021/2022 vikao vitatu (03) vimefanyika.
Vikao na wadau. Mkakati wa ofisi kwa mwaka 2021/2022 ni kufanya vikao vinne na kufikia Mei 2022 vikao viwili vimefanyika
Ziara shuleni. Katika mwaka 2021/2022 ofisi imetembelea shule 26 na jumla ya walimu 218 wamefikiwa.