RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMTEUA PROF. MURUKE KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU

16 May, 2024
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMTEUA PROF. MURUKE KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Masoud Hadi Muruke kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Prof. Muruke anachukua nafasi ya Prof. Willy Lazaro Komba ambaye muda wake umemalizika.

Taarifa ya uteuzi huo ilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus tarehe 15 Mei, 2024.