Kanuni Na. 5 (1) – (5) ya Kanuni za Utumishi wa Walimu za mwaka 2016 zimeelekeza utaratibu wa kuwathibitisha kazini Walimu ambao wamemudu majukumu ya kazi na kuwaondoa kazini Walimu ambao wameshindwa kumudu majukumu (hawajakidhi vigezo) baada ya kumaliza muda wa matazamio (Probationary Period) uliowekwa kisheria.
Ufuatao ni utaratibu wa kuwathibitisha kazini Walimu ulioainishwa kwenye Kifungu hicho;
i. Mwalimu anapaswa kuthibitishwa kazini ndani ya miezi 12 tangu alipoajiriwa kwa mara ya kwanza kwenye Utumishi wa Umma;
ii. Miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha matazamio, Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika itapeleka mapendekezo kwenye Tume ngazi ya Wilaya. Tume ngazi ya Wilaya itayachambua na kuyawasilisha kwenye Kikao cha Kamati ya Wilaya ambayo itatoa uamuzi iwapo Walimu wamekidhi vigezo vya kuthibitishwa, au kipindi cha matazamio kiongezwe ili kumpa Mwalimu nafasi ya kujirekebisha au ajira yake isitishwe. Mwalimu atajulishwa kwa barua juu ya uamuzi uliofikiwa. Iwapo Mwalimu atakuwa ameongezewa muda wa kipindi cha matazamio, muda huo haupaswi kuzidi miezi sita (6); na
iii. Tume ngazi ya Wilaya watatoa barua za kuwajulisha Walimu uamuzi uliofikiwa na Kamati;
Kuthibitishwa kazini kunamwezesha Mwalimu kupata stahili nyingine za kiutumishi ikiwemo kupandishwa cheo na au kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Secretary PO-TSC
Postal Address: P. o Box 353 DODOMA
Telephone: +255 26 2322402
Mobile:
Email: secretary@tsc.go.tz
Copyright ©2017 TSC . All rights reserved.